Posts

Showing posts from October, 2017

aS Roma matatani

Image
Klabu ya Roma imeshitakiwa na UEFA baada ya baadhi ya mashabiki wake kusikika wakiimba nyimbo zenye ujumbe wa ubaguzi wa rangi kwa kumwita Nyani mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani aliingia dakika ya 77 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa siku ya Jumatano ambapo mchezo huo ulimalizika kwa matokeo ya 3-3 kwenye dimba la Stamford Bridge. Kesi hiyo itasikilizwa na kutolewa maamuzi Novemba 16 mwaka huu na Kamati ya UEFA ya Udhibiti wa Maadili na Nidhamu. Rudiger, mwenye umri wa miaka 24, amehamia Chelsea kutoka Roma kwenye usajili wa majira ya joto mwaka huu. Kabla ya kuhamia Uingereza kwa gharama ya £ 29m, Rudiger alisema ubaguzi wa rangi katika mechi za mpira wa miguu ni tatizo kubwa nchini Italia.

TOP SCORERS KWENYE LIGI KUU YA ENGLAND

Image

Seven matches down, the #PL table as it stands...

Image

Serikali yampiga marufuku msanii Bobi Wine kufanya interview

Image
Tume ya mawasiliano nchini Uganda (UCC) imepiga marufuku kwa vyombo vya habari nchini humo kufanya 'interview' na mwanamuziki Bobi Wine, baada ya kuonekana kinara kwenye suala la kupinga ukomo wa urais nchini humo. Taarifa hiyo imetolewa na mwenyewe Bobi Wine ambaye pia ni mbunge wa upinzani nchini humo kwenye ukurasa wake wa instagram akisema kuwa amepigiwa simu na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo na kuthibitisha suala hilo, kuwa wamepigwa marufuku kufanya naye mahojiano yoyote. "Hii asubuhi nilitakiwa kufanya mahojiano na Capital FM, baadaye nikataarifiwa kuwa wamepewa agizo na UCC na kupigiwa simu na watu wa usalama kwamba wasiwe na mimi, nikapigiwa simu na vituo vingine vya redio na runinga na kunithibitishia wamepewa agizo hilo hilo na kwa vitisho, na iwapo watakuwa na mimi watakuwa katika hatari ya kufungiwa", ameandika Bobi Wine. Bobi Wine ameendelea kuandika akisema kwamba.. "Iwapo unaangalia dalili za kuanguka kwa serikali usiendelee tena, huu...